simbasc_breaking_news on Instagram

Mwana Msimbazi 🦁🦁

OFFER πŸ€— TANGAZA PAGE YAKO NA BIASHARA πŸ‘‰ DM UPDATE za Simba πŸ”₯ Update za VPL πŸ”₯ PIA TUPO TELEGRAM BONYEZA LINK KWENYE BIO

https://t.me/joinchat/NfGAw1BhGYB6Lk3xCJQX8w See full size profile picture

Report inappropriate content

@simbasc_breaking_news photos and videos

#NguvuMoja

1

Ikiwa ndio baadhi ya wachezaji wanaelekea kumaliza mikataba yao na Dirisha la usajili la msimu wa joto linakaribia, Shirikisho la Kandanda Ulimwenguni FIFA limetoa ufafanuzi zaidi kwamba mkataba wa mchezaji utamalizika kwenye klabu yake pale tu msimu wa Ligi utakapomalizika. Kwasasa ikumbukwe kwamba ligi kadhaa Ulimwenguni zimesimama kutokana na mlipuko wa virusi vya Corona na ligi mbalimbali zilitaraji kuhitimishwa mwezi ujao wa Mei Hivyo ni wazi mkataba wa wachezaji na klabu yake utahesabika kwamba utamalizika pale tu msimu wa ligi utakapo kuwa umemalizika. Wakati huohuo pia FIFA Imethibitisha kuwa dirisha la usajili msimu wa majira ya joto litaendelea zaidi ya Juni 30 ikiwa ni mapendekezo yaliyokubaliwa na wadau wote pamoja na viongozi wa mpira. #NguvuMoja #thiissimba #sisinisoka

0

Afisa Habari na Msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara amesema masuala yanayohusu uwekezaji kwenye klabu hiyo yanawahusu Wanachama na Mashabiki wa Simba Siku za karibuni baadhi ya vyombo vya habari hasa redio zimekuwa zikiendesha vipindi vya mijadala ambapo moja ya mijadala hiyo ilihoji hatma ya Bilioni 20 ambazo mwekezaji wa klabu ya Simba Bilionea Mohammed Dewji 'Mo' aliahidi kuziweka kwenye akaunti ya mabingwa hao wa nchi baada ya mchakato mzima wa uwekezaji kukamilika Manara amesema kimsingi wapenzi, wanachama na mashabiki wa Simba ndio wenye uhalali wa kuhoji masuala yanayoihusu klabu yao na sio kila mtu afanye hivyo kwa utashi wake "Wenye uhalali wa kuhoji kuhusu Bilioni 20 za mwekezaji wa Simba ni mashabiki wenyewe ambao walimpa timu, siyo mtu mwingine tu ambaye hana uhalali," Manara aliiambia EA radio Mo alishinda zabuni ya uwekezaji kunako klabu ya Simba mwaka 2017 akinunua hisa asilimia 49 kwa kiasi hicho cha fedha Tangu wakati huo Mo amekuwa ndiye msimamizi mkuu wa klabu ya Simba akilipa mishahara ya wachezaji pamoja na kununua wachezaji wapya #NguvuMoja

9

Kiungo wa Simba Jonas Mkude amesema kuwa endapo Ligi Kuu Bara itaendelea baada ya muda wa kusimama, kutakuwa na changamoto mbalimbali kwa wachezaji kurejea kwenye ari ya mchezo ikiwamo suala la kukosa pumzi na majeraha Mkude ametoa kauli hiyo wakati huu kukiwa bado haifahamiki ni lini ligi itarejea kutokana na changamoto ya ugonjwa wa Corona Fundi huyo wa mpira amesema changamoto kubwa anayoiona iwapo wachezaji watarejea ni kwamba wengi wao watakabiliwa na suala la uwiano tofauti wa pumzi ikiwamo baadhi yao kukata mapema, jambo ambalo litaziathiri timu nyingi katika juhudi za kusaka ushindi. Aidha, Mkude aliongeza kuwa kutokana na kila mtu kufanya mazoezi kivyake haamini kama kila mmoja anajibidiisha kuyafanya ipasavyo huko aliko kwa sasa. Ligi mbalimbali za soka duniani zimesimama kupisha juhudi za kukabiliana na ugonjwa wa corona ambao umekuwa changamoto na kusababisha mambo mengi kusimama. #NguvuMoja

1

Kocha mkuu wa timu ya Simba, Sven Vandenbroeck ameliomba Shirikisho la soka Tanzania (TFF) liwape muda wa wiki mbili kujiandaa ligi ikirejea baada ya kumalizika kwa mlipuko wa homa ya virusi vya Corona. Mbelgiji huyo amesema anafahamu wachezaji hawatakuwa na muunganiko sawa kwakua watakuwa hawajapata muda wa kufanya mazoezi ya pamoja kutokana na kusimama kwa ligi. Ligi kuu ya Vodacom Michezo yote nchini imesimama kwa wiki ya tatu sasa kutokana na mlipuko wa homa ya virusi vya Corona ambayo inazidi kutikisa dunia kila kukicha. "Nadhani tunahitaji kupewa wiki mbili za kujiandaa kufanya mazoezi ya pamoja baada ya hali kuwa shwari ili wachezaji wawe na muunganiko na ushindani uwe mkubwa kama ilivyokuwa mwanzoni," alisema Sven. Mpaka ligi hiyo inasimama Simba ilikuwa ipo kileleni mwa msimamo ikiwa na pointi 71 baada ya kucheza mechi 28 ikisalia na michezo 10. #NguvuMoja

2

Mlinzi wa kutumainiwa ndani ya kikosi cha Simba, Mohamed Hussein β€˜Tshabalala’ amesema anajivunia kuwa miongoni mwa wachezaji ndani ya kikosi bora cha Simba. Tshabalala miongoni mwa nyota wenye nidhamu ya hali ya juu ndani na nje ya uwanja ana uhakika wa namba ndani ya kikosi chake licha ya kuwa na ushindani dhidi ya mkali mwenzie, Gadiel Michael, aliyetua kutoka kwa mahasimu, Yanga. Nahodha huyo msaidizi amesema anajisikia faraja kuwa sehemu ya kikosi cha mabingwa hao wa Tanzania Bara "Nafurahi kuwa hapa na pia kwangu mimi ni heshima kubwa kuchezea Simba, nitazidi kupambana kuhakikisha nakilinda kiwango changu ili nizidi kupata namba chini ya kocha yoyote atakayeinoa Simba," amesema Aidha Tshabalala anasema, katika kumbukumbu za maisha yake katika soka, hatasahau kuwa alikuwa sehemu ya wachezaji walioipeleka Simba hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika. "Hili jambo halitafutika maishani mwangu, ni historia na itakuwa kumbukumbu yangu maishani" Nyota huyo amesisitiza mafanikio ambayo klabu yake inayapata yanatokana na umoja uliopo ndani ya timu yao kuanzia viongozi, wachezaji mpaka mashabiki wao. #NguvuMoja

5

Kocha Msaidizi wa klabu ya Simba, Selemani Matola, amesema upo ugumu kuwafuatilia wachezaji kwa wakati huu kama wanafanya mazoezi au la katika kipindi hiki ambacho virusi vya Corona vimesitisha shughuli zote za michezo duniani Corona imesababisha shughuli za soka duniani kote kusimama, ikiwemo Ligi Kuu Tanzania Bara, ikiwa ni agizo la serikali la kusimamisha shughuli zote za kuzuia mikusanyiko lililotolewa mwezi uliopita. Matola amesema kwa sasa sio rahisi kuwafuatilia wachezaji mmoja mmoja kubaini kama wanafanya mazoezi au la "Kwa sasa ni ngumu kujua kwamba wachezaji wanafanya mazoezi ama la kutokana na mfumo wa maisha kuwa tofauti na kila mmoja kuwa na mtindo wake mwenyewe", amesema Matola. "Kinachotakiwa ni kwa kila mchezaji kuwa makini kufanya yale aliyoelekezwa ili awe bora na imara pale ligi itakaporejea", ameongeza kocha huyo ambaye pia aliwahi kuwa mchezaji wa klabu hiyo. Maoni ya Matola yanaakisi kile kilichosemwa na kocha mkuu wa mabingwa hao wa nchi Sven Vandenbroeck ambaye amependekeza TFF kuvilabu vilabu angalau wiki mbili za kujifua pale ligi itakaporejea Hatma ya mshikemshike wa ligi kuu kuendelea inasubiri uamuzi wa Serikali kulingana na mwenendo wa maambukizi ya virusi vya Corona #NguvuMoja

1

πŸ“· Edit πŸ’― πŸ˜€πŸ˜€ πŸ˜‚πŸ˜‚ Nini maoni Yako asajiriwe au No? Follow @saimon_simba #NguvuMoja #thisissimba #yeswecan #michezo #hainakufeli

24

Apo kuna Jezi na Kanzu πŸ˜‚πŸ˜‚ @saimon_simba

2

Rekodi zipo sawa. Tunashikilia rekodi ya kupindua matokeo katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuifunga Mufulira Wanderers ya Zambia mabao 5-0. Mchezo wa awali uliopigwa hapa nchini tulipoteza kwa mabao 4-0. Hiyo ilikuwa hatua ya kwanza ya #TotalCAFCL mwaka 1979. πŸ’ͺ🏽🦁 πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€kwani CAF hawana historia za utoporo pia? Mi najua hili litaleta tatizo kwa mtani wetu, watasema tunapendelewa mpaka CAFπŸ˜ƒπŸ˜ƒ 🐸🐸 #NguvuMoja

0

🀣🀣🀣 follo @saimon_simba kwa vichekesho

13